Header Ads

Iraq imewahukumu adhabu ya kifo wanawake 15 raia wa Uturuki,



MAHAKAMA nchini Iraq imewahukumu adhabu ya kifo wanawake 15 raia wa Uturuki, baada ya kupatiakana na hatia ya kujiunga na kundi la kigaidi la Islamic State (IS).
Kuna taarifa kuwa, baadhi ya wanawake hao wamehukumiwa kifo, wengine walihukumiwa kifungo cha maisha.
Wanawake hao wamekiri kuolewa na wapiganaji wa Islamic State au waliwasaidia kufanya mashambulizi ya kigaidi.
Maelfu ya raia wa kigeni wamepigana na kuuliwa wakiwa na wapiganaji wa IS nchini Iraq na Syria.
Serikali ya Iraq imatangaza kumalizika kwa vita na kundi hilo Desemba mwaka jana.
Licha ya IS kutimuliwa kutoka ngome zake kuu, kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga na mashambulizi mengine.
Wanawake hao wanaotajwa kuwa kati ya umri wa miaka 20 hadi 50, walikuwa wamevalia nguo nyeusi wakiwa mahakamani mjini Baghdad, wanne kati yao walikuwa na watoto wadogo.
Katika kujitetea, mmoja wa wanawake hao, alidai mbele ya Mahakama kuwa alishiriki katika vita dhidi ya wanajeshi wa Iraq akiwa na kundi na IS.
Takriban wanawake 560 na watoto 600 wanashikiliwa na serikali ya Iraq kwa tuhuma za kuhusishwa na matukio ya kigaidi au kuwa na undugu na wapiganaji wa IS.
Mapema mwezi huu, mwanamke raia wa Uturuki alihukumiwa adhabu ya kifo na wengine 10 wakahukumiwa kifungo cha maisha 

No comments