SPORTPESA YAZINDUA KITUO KIKUBWA
SPORTPESA YAZINDUA KITUO KIKUBWA
Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa Tanzania jana imezindua rasmi Kitengo cha Huduma kwa Wateja katika kuboresha huduma kwa wateja.
SportPesa kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Utawala na Udhibiti, Tarimba Abbas kitengo hicho maalumu cha huduma kwa wateja kilikuwa kikiendesha shughuli zake nchini Kenya yalipokuwa makao makuu.
“Ili kuboresha zaidi huduma zetu tumehamisha kitengo chetu cha huduma kwa wateja katika ofizi zetu za hapa jijini Dar es Salaam ili kuonyesha jinsi gani tunawajali na kuwafikiria wateja wetu kwa kusogeza huduma karibu yao.
“Kutokana na moja ya changamoto ambazo vijana wanapitia kuwa ni ajira, sisi kama SportPesa tumeajiri vijana wapatao 84 kwenye kitengo chetu na hawa wamefanyiwa mafunzo jinsi ya kuwasilikiza na kuwahudumia wateja kwa uzoefu wa hali ya juu.
“Kama mnavyojua sisi tutakuwa ni kampuni ya kwanza ya michezo ya kubashiri yenye huduma kwa wateja wake kwa saa 24 kwa siku saba za wiki, hii inaonyesha ni namna gani mteja wwetu ni kipaumbele namba moja,”alisema Tarimba.
Aidha, Tarimba aliwaomba Watanzania kuiunga mkono kampuni hiyo ambayo imedhamiria kuleta sura mpya kwenye sekta ya michezo nchini sambamba na kubadilisha maisha ya Mtanzania kupitia programu mbalimbali ikiwa ni promosheni ya siku 100 ya TVS King Deluxe.
Post a Comment