Header Ads

Waumini wakanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania E.A.G.T KANANI mwanza road, waobwa kuwa watii


 Waumini wakanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania E.A.G.T KANANI  mwanza road, waobwa kuwa watii

Related image

Waumini wakanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania E.A.G.T KANANI  mwanza road, waobwa kuwa watii kwa kila jambo lolote  ili wafanikiwe katika maisha yao kama maandika matakatifu yanavyo elekeza kutoka kwenye biblia.


Akizungumza kwenye ibada takatifu iliyo fanyika  katika kanisa la KANANI E.A.G.T, mchungaji DASHONI JERADI kutoka kanisa la mwanzungi E.A.G.T wilaya ya igunga aliyasema maneno hayo alipokuwa akiubili neno la mungu hivyo aliwahasa waumini kuwa watii kama biblia inavyo eleza ili wafanikiwe katika maisha yao ya kiroho na kimwili akinuku  andiko kutoka katika kitabu takatifu  cha biblia ISAYA 1.19.

Bw JERADI aliwahasa  waumini  wa kanisa la KANANI E.A.G.T kuwa watii wakiwa sehem yoyote hata wakiwa kwenye kazi zao ili wafanikiwe kwani utii umpa mtu nafasi kubwa kwa mwajili wake hivyo yatu pasa kuwa watii kama alivyo kuwa mwokozi mwetu bwana yesu kristo alivyo kuwa akiangizwa na mungu aliyafanya yote na hata akafa msalabani kwajili yetu iliaje atukomboe na sasa tupo huru nasisi yatupasa tuwe watii kama mwokozi wetu ili tupate kibali  machoni pa  mungu na wanadam .


Aidha aliwataka waumini kuto changua watu ambao wa kuwatii bali wawatii hata wale ambao  hawaja mwamini yesu kuwa mwokozi wao ili wajifunze kutoka kwa walio okoka kwani watu wamungu ni barua kilamtu anaisoma hivyo yatupasa kumcha mungu na kutunza wokovu wetu ili bwana yesu atapo kuja atukute tukiwa safi katika miyo yetu.

No comments