Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, mradi huo utasaidia kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi
Kwa mujibu wa Makamu wa Rais, mradi huo utasaidia kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi na kuchochea ukuaji wa sekta hiyo Nyanda za Juu Kusini kwani vivutio vyake havijapewa kipaumbele cha kutosha kama vile vya maeneo ya kaskazini mwa nchi.
Amesema, mradi huo wa miaka sita, unatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia, utasaidia kukuza miundombinu kama viwanja vya ndege, kuhifadhi mazingira na kusaidia jamii ya watu walioko kando mwa hifadhi za wanyama.
Mwakilishi wa Benki ya Dunia, Bella Bird asema kuwa Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vya utalii bora duniani na kuongeza mradi wa REGROW utasaidia kukuza sekta ya utalii na kwa kuongeza idadi ya watalii nchini.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala amesema kuwa moja ya changamoto zinazoukabili ukanda wa kusini ni ujangili kwani kuna wananchi wanaodiriki kutumia sumu kuua wanyamapori, hususani tembo.
Post a Comment