Header Ads

Madhara ya kahawa katika mwili wa binadam

Madhara ya kahawa katika mwili wa binadam                         

Image result for hasara ya kutumia kahawa


 kunywa kahawa imekua moja ya ni moja ya tamaduni zetu kwenye maisha ya kila siku, kahawa inatumika na jamii nyingi duniani.
hapa kwetu tanzania kahawa inatumika majumbani na hata vijiweni utawakuta watu wanatembeza kahawa na kashata, wateja wa huduma hii ni wengi sana.

kahawa inafanya kazi gani kwenye mwilini?

Image result for hasara ya kutumia kahawa


kemikali iliyopo ndani ya kahawa ya caffeine kitaalamu inaitwa 1,3,7-trimethyxanthine, kwa hali ya kawaida kahawa inakua kama unga mweusi mchungu sana lakini hupelekwa viwandani na kubadilishwa na kuongeza vionjo.
ukinywa kawaha baada ya dakika kumi huingia kwenye damu na kusafiri mpaka kwenye ubongo, huko hubadilisha hali ya mtu kutoka kwenye utulivu na kumfanya achangamke.
kahawa huzuia kemikali moja kitaalamu kwa jina la adenosine, kwa hali ya kawaida adonenosine huzuia kemikali ya uchangamfu kwa jina la acetycholine.

kahawa pia humwaga homoni za adrenaline kwenye damu, homoni hizi hua zinatengenezwa mtu akiwa na wasiwasi, uoga, hasira au akitaka kupigana.
sigara inaongeza kasi ya kazi ya kahawa mwilini hivyo wavuta sigara wakinywa kahawa inawaingia haraka kuliko watu ambao sio wavutaji.

unywaji wa kahawa huleta faida za muda tu ambazo ni kama kuondoa usingizi na kukufanya usome au ufanye kazi kwa muda mrefu, huondoa uchovu na uvivu unapoinywa, ni nzuri kwa wagonjwa wa pumu kwani hupanua mirija ya hewa, watu wengine huweza kuondoa maumivu ya kichwa kwa kunywa kawaha, kimsingi dawa nyingi za kutuliza maumivu zina kemikali ya caffeine inayopatikana kwenye kahawa.

pamoja na faida zote hizo kahawa ina madhara ambayo ni hatari kwenye mwili wa binadamu kama ifuatavyo.
huongeza sukari mwilini; kemikali ya caffeine inayopatikana kwenye kahawa huongeza sukari mwilini kwa kuongeza kiwango cha adrenaline, hii ni hatari sana kwa mgonjwa mwenye kisukari tayari.

huongeza kukojoa; kahawa hufanya mtu kukojoa mara kwa mara kitaalamu kama diuresis hii huweza kuleta usumbufu mkubwa wakati wa kulala au wakati wa kazi.

huongeza kiwango cha lehemu au cholestrol mwilini; cholestrol hatari mwilini kwa jina la lower density lipoprotein[ldl] huongezeka kwa asilimia tano kwa matumizi ya kahawa.

hupunguza kasi ya mmengenyo wa chakula; kemikali ya cafein hufunika eneo la tumbo kwa kuweka kitu kama koti na kuzuia mmengenyo mzuri wa chakula, magonjwa mbalimbali ya tumbo kama colitis huongezwa zaidi na kahawa.

kukosekana kwa vitamin b; caffeine hupotea pale kahawa inapotumika kwa wingi sana, hupunguza vitamin b ambayo ni muhimu sana kwenye kuvunja wanga na kuupa mwili nguvu.

huleta madhara kwenye moyo; kemikali ya caffaine husababisha moyo kupiga bila mpangilio maalumu, hii ni huweza kusababisha mshituko wa moyo hasa kwa wagonjwa wa moyo.

kukosa usingizi; kahawa huharibu ubora wa usingizi, hii humfanya mtu kulala kwa kuhangaika sana huku ukaimaka mara kwa mara katikati ya usingizi, mara nyingi wanafunzi wanaotaka kusoma muda mrefu usiku hunywa kawaha kupata hii kitu.

humaliza nguvu za mwili; ukinywa kahawa unaufanywa mwili ushindwe kupumzika kipindi unafanya kazi hivyo unakua una nguvu sana mwanzoni, baadae kahawa ikiisha mwilini mtu hujikuta na uchovu mkali sana.

hupunguza kiasi cha madini ya kashiamu mwilini; matumizi ya kahawa huufanya mwili kuondoa kiasi kikubwa cha kashiumu kupitia mkojo na choo kubwa na kusababisha kukosa kiasi kikubwa cha kashiumu mwilini, hii huweza kuleta magonjwa ya mifupa kama kuvunjika na matege kwa watoto.

huongeza kiasi cha tindikali tumboni; kahawa husababisha kutengeneza kwa kiasi kikubwa mno kwa tindikali ambayo hupatikana tumboni kwa ajili ya kumengenya chakula, tindikali hii ikiwa nyingi husababisha mmengenyo mbovu wa chakula na maumivu makali kwa watu wenye madonda ya tumbo

kuchosha figo na maini; sababu kemikali ya caffaine inafanyisha kazi sana viungo hivi vya mwili baadae viungo hivi huchoka sana na kupoteza ufanisi, hii ndio sababu wagonjwa wa ini na figo hushauriwa kutotumia kahawa.

madhara kwa mtoto anayenyonya; kunywa kahawa zaidi ya miligram 200 huweza kupita kwenye maziwa na kwenda kwa mtoto, kunywa kahawa kipindi cha ujauzito huweza kuleta upungufu wa damu kwa mama na mtoto.

vipi kuhusu chai ya rangi nyeusi?
japokua chai ya rangi ina kemikali ya caffaine kama kahawa ila kiasi chake ni kidogo sana kwenye chai, chai faida mbalimbali kama kuua bacteria na virusi mbalimbali mdomoni japokua chai ikitumika na chakula hapohapo huzuia mwili kupata madini kama kashiumu,madini ya chuma na zinki na pia ina madhara kama ya kahawa.
chai pai ina kemikali ya floride ambayo huimarisha meno, na husafisha mdomo.

je kitu gani ni bora kutumika mbadala wa chai nyeusi na kahawa?

Image result for hasara ya kutumia kahawa

chai ya kijani maarufu kama green tea ni nzuri sana kwa mwili wa binadamu...hupunguza presha ya damu,kuipa nguvu mishipa ya damu,hutibu magonjwa yasababishwayo na bacteria na kuzuia damu kuganda.
kutumia kahawa na chai nyeusi ambazo zimeondolewa kemikali ya caffeine ni vizuri lakini pia chai kwa jina la herbal tea ni nzuri sana kiafya 

kumbuka mwili ni afya jali sana afya yako linda mwili wako kwa kula vyakula vyenye nguvu mwilini,,,,,tumia matunda 

Image result for matunda





No comments