JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka wanafunzi wa vyuo na sekondari, kujitayarisha kuwatumikia wananchi
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka wanafunzi wa vyuo na sekondari, kujitayarisha kuwatumikia wananchi
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka wanafunzi wa vyuo na sekondari, kujitayarisha kuwatumikia wananchi na wasifi kirie kwamba watakapoajiriwa mahakamani watatajirika.
Aidha, alisema kazi ya Mahakama inahitaji watumishi wenye maadili na uadilifu wa hali ya juu kwa kuwa utoaji wa haki unagusa maisha na uhai wa watu, kusababisha watu kufilisika, kusimamisha uwekezaji na wengine kupoteza kazi. Jaji Profesa Juma alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na walimu na wanafunzi kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria.
Alisema kumekuwa na malalamiko ya kuporomoka kwa maadili kutokana na vitendo vya rushwa na kwamba mikakati imewekwa kupambana na tatizo hilo. “Tumeona tutoe elimu kuhusu Mahakama kwa kuwa mnapokuwa shuleni na vyuoni mnatayarishwa tu, lakini dunia ya sasa imebadilika watu mnatakiwa kusoma bila Mwalimu kwani Tanzania ijayo si sawa na iliyopita kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, ushindani na uelewa wa hali ya juu,” alisema Profesa Juma.
Alifafanua kuwa watu hawajajitokeza kutoa ushahidi kuhusu masuala ya rushwa ili wanaofanya vitendo, hivyo wachukuliwe hatua, hali ambayo inaongeza ukiukwaji wa maadili. “Utakumbuka mwaka 1996 Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba aliwasilisha ripoti kuhusu rushwa inavyofanyika nchini lakini mpaka sasa bado tunaendelea kukemea hali hiyo.
Post a Comment