Israei yatoa ilani kwa maelfu ya wahamiaji wa kiafrika imewataka waondoke kufikia mwezi Machi
Israei yatoa ilani kwa maelfu ya wahamiaji wa kiafrika imewataka waondoke kufikia mwezi Machi
Israei yatoa ilani kwa maelfu ya wahamiaji wa kiafrika
imewataka waondoke kufikia mwezi Machi. Maafisa wanasema kwamba endapo
onyo hilo halitotekelezwa wahamiaji huenda wakajikuta wakikamatwa na
kufungwa jela.
Israel imeanza kutoa onyo kwa maelfu ya wahamiaji wa kiafrika tangu
hapo jana ikiwataka waondoke nchini humo kufikia mwezi Machi. Maafisa
wanasema kwamba endapo onyo hilo halitotekelezwa wahamiaji huenda
wakajikuta wakikamatwa na kufungwa jela.
Maafisa nchini Israeli
wameshaanza hatua ya kugawa vikaratasi vya ilani kwa wahamiaji wa
kiafrika kuanzia hapo jana wakitakiwa kufunganya virago kwa khiari na
kuiaga nchi hiyo chini ya mpango maalum unaolenga kuwaondowa kiasi watu
38 elfu wanaoomba hifadhi katika taifa hilo la Mashariki ya Kati,
amesema msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Israel.
Ilani hiyo
inayotowa muda wa miezi miwili kwa wahamiaji kuondoka inatajwa kwamba
inatolewa kwa wanaume wasiokuwa na watoto. Serikali ya Israel inawataja
waomba hifadhi walioko nchi humo kuwa ni wahamiaji wanaotafuta maslahi
ya kiuchumi ikiwaita kwamba ni watu waliojipenyeza nchini humo.
Hivi karibuni waziri mkuu Netanyahu alisikika akisema:
Watu waliojipenyeza kinyume cha sheria nchini wana chaguo
rahisi-ama kutoa ushirikiano na sisi na kuondoka kwa khiari,kwa heshima
na kihalali au tutalazimika kutumia njia nyingi zilizoko kwenye uwezo
wetu,na ambazo pia ziko kisheria.Nataraji kwamba wataamua kushirikiana
nasi.''
Waziri mkuu Netanyahu akiwa Uganda na rais Museveni Julai 2016
Kwa
mujibu wa mpango wa Israel wahamiaji watakaoamua kuchagua kuondoka kwa
khiari watapewa dolla 3,500 pamoja na tiketi ya ndege ya kwenda nchi
nyingine ambayo haikutajwa. Wanawake ,watoto na kina baba wanaotegemewa
na watoto wao hawaguswi katika mpango huo. Hata hivyo kuanzia mwezi
Aprili kiwango cha dolla 3500 zinazotolewa kitapunguzwa taratibu na
endapo kuna mhamiaji aliyeamua kubakia katika nchi hiyo atakuwa katika
uwezekano wa kufungwa jela.Wengi wa wakimbizi wanasema wanakhiari
kufungwa kuliko kurudishwa barani Afrika. Uamuzi wa Isreal umekosolewa
na mashirika mbali mbali ya kutetea haki za binadamu.
Tamara
Newman, mkurugenzi wa mahusiano ya kimataifa katika kitengo maalum
kinachowashughulikia wakimbizi na wahamiaji Israel anasema:
''Mpango
wa Israel wa kuwaondoa waomba hifadhi 38,0000 kuwapeleka Rwanda pasipo
khiari yao ni kitu kisichokubalika kabisa katika nchi yenye demokrasia
ambayo imetia saini makubaliano ya kimataifa kuhusu wakimbizi. Serikali
inawaambia wahamiaji sasa kwamba wana njia mbili za kuchagua ama
kupelekwa Rwanda au kutiwa jela kwa kipindi kisichojulikana. Hili sio
chaguo la kweli.tafiti zote zimetuonesha kwamba wote waliopelekwa Rwanda
maisha yao yamezidi kuwa hatarini''
Wengi wa watu wanaoomba
hifadhi nchini Israel wanaokabiliwa na hali hiyo ya kuondolewa kwa
nguvu ni raia wa Sudan na Eretrea. Kadhalika Uganda na Rwanda zinatajwa
kwamba ni nchi ambazo wakimbizi hao huenda wakapelekwa ingawa nchi hizo
zimekanusha kuwa ni vituo vya kuwapokea wahamiaji watakaorudishwa
Afrika kutoka Israel.
chanzo dw swahili
Post a Comment