Header Ads

Rais John Magufuli amemwapisha Dk Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi

Rais John Magufuli amemwapisha Dk Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kabla ya uteuzi, Dk Kilangi alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kampasi ya Arusha, pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Mafuta, (Tanzania Petroleum Upstream Regulatory Authority- PURA).
Naibu Mwanasheria Mkuu Paul Ngwembe kabla ya uteuzi, alikuwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA). Kabla ya kuwa Mwansheria Mkuu wa Serikali, George Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu akiongozwa na Mwansheria Mkuu, Fredirick Werema.

No comments