Header Ads

Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA limesema leo kuwa lina imani kubwa katika hatua zake za usalama

Image result for fifa


Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA limesema leo kuwa lina imani kubwa katika hatua zake za usalama 

zitakazowekwa wakati wa dimba la Kombe la Dunia nchini Urusi. Hii ni baada ya suala la uhuni wa mashabiki wa taifa hilo mwenyeji kujitokeza upya kufuatia matukio kadhaa ya vurugu yaliyowahusisha mashabiki wa klabu ya Spartak Moscow jana usiku ambapo polisi mmoja aliuawa kutokana na mshtuko wa moyo. Askari huyo alifariki katika hospitali ya mji wa kaskazini mwa Uhispania wa Bilbao.

 Polisi walikabiliana na mashabiki wa Spartak na Athletic kabla ya mchuano wa Europa League jana. FIFA imesema kuwa ina inaamini kabisa mipango yake ya usalama iliyowekwa na maafisa wa Urusi na Kamati ya Maandalizi. Imesema hilo lilidhihirika wazi wakati wa mashindano ya mwaka jana ya Kombe la Mashirikisho la FIFA yaliyoandaliwa Urusi.

No comments