Header Ads

Atokwa funza sehemu za siri kisa mke wa mtu

Mwanaume mmoja amekutwa na balaa la kutokwa na funza sehemu za siri, 
baada ya kuiba mke wa mtu ambaye ni mke wa bosi wake, huko Kaunti ya Busia
 nchini Kenya.

Akizungumza kwa sauti ya kulia huku akiomba msamaha, mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa, alisikika akimsihi bosi wake aliyejulikana kwa jina la Mr. Ouma amsamehe kwa alichofanya na kuapa kutorudia, huku akionyesha namna wadudu hao wanavyotoka kwenye sehemu zake za siri.
“Mama nisaidie nakufa, nakubali nimefanya, nisamehe ndugu yangu, siwezi rudia mara nyingine, ndugu yangu nisaidie”, alisikika mwanaume huyo akimsihi bosi wake.
Kwa upande wa bosi wake huyo amesema kuwa alimuajiri mwanaume huyo kufanya kibarua cha kupalilia shamba, lakini alijiongeza na kujipa kibarua cha kulala na mke wake, na alishamuonya lakini hakutaka kusikia na kuzidi kuendelea mpaka siku moja alimfuma kitandani kwake akiwa na mkewe.
“Mimi nilienda safari lakini nikaambiwa kuhusu wao, nikakaa kimya, siku moja nikamkuta kitandani kwangu na mke wangu, mke wangu akaondoka kwenda naye kwake, yeye mwanaume akaniambia wewe huwezi kazi ya nyumba, nikashtuka sana kuniambia hayo, nikipiga simu ya mke wangu yeye ndio anapokea, nikaenda kwa mganga nikataka kuwapa fundisho”, amesema Mr. Ouma ambaye mmiliki wa mke.
Baada ya tukio hilo Mr. Ouma alimleta mganga ambaye alimfuata mara ya kwanza kumtibia mwizi huyo, na hatimaye kupona na wadudu kuuacha kutoka, na kumuacha mke wake hapo hapo.

kilicho fanyika tabora



No comments