Header Ads

mpango wa ndege za kivita Ujerumani na Ufaransa



ILA Air Show in Berlin 2018 | Florence Parly & Ursula von der Leyen (Reuters/)


Ujerumani na Ufaransa zimekubaliana kuhusu mahitaji makuu kwa ajili ya ndege mpya ya kivita kuchukuwa nafasi ya Typhoon ya Eurofighter na Rafale kuanzia 2040, kulingana na duru za wizara ya ulinzi ya Ujeurmani
Hatua hii itaanzisha mradi uliozinduliwa kwa mara ya kwanza Julai mwaka jana na maafisa kutoka mataifa yote mawili watasaini waraka wa uainishaji kandoni mwa maonyesho ya ndege za kivita ya Berlin ILA, yaliofunguliwa na kansela Angelea Merkel siku ya Jumatano. 
Pamoja na kuwa na uwezo wa kufanyakazi kivyake, au kuongoza kundi lingine la ndege zikiwemo zisizo na rubani, ndege hiyo itahitaji pia kuwa na uwezo wa kuendesha operesheni za mashambulizi na kujihami, walisema maafisa wa wizara ya ulinzi ya Ujerumani.
Ilikuwa haijaamuliwa bado iwapo ndege hiyo mpya itakuwa inaendeshwa tu na rubani au itakuwa pia na toleo la isiyokuwa na rubani. Lengo ni kuanza kuzitumia ndege hizo mpya, zikiwa na uwezo wenye mipaka, kuanzia mwaka 2040.

sikiliza hapa chini sylas tv


No comments