Header Ads

Mafuriko yauwa 15 nchini Kenya



Image result for Mafuriko yauwa 15 nchini Kenya

Msimu mrefu ambao si wa kawaida wa mvua umeathiri maeneo kadhaa ya Kenya , huku kukiwa na ripoti kwamba zaidi ya watu 15 wamefariki katika nchi hiyo kutokana na mafuriko. Barabara kuu kadhaa zimeharibika na kusababisha wasafiri wengi kushindwa kusafiri kwa masaa kadhaa wakati biashara nchini humo pia zimeathirika kutoka na mvua hizo kubwa. 

Mkaazi wa mjini Nairobi, Bernad Mokera, amelalamikia mfumo usiofaa tena wa mifereji unaosababisha mafuriko na kutoa wito kwa maafisa kufanyia kazi suala hilo. Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya , mvua kubwa na mafuriko zinatarajiwa kuendelea kwa siku kadhaa zijazo.

angalia hapa chini 

No comments