Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajadili iwapo kulipigia kura pendekezo la Marekani
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linajadili iwapo kulipigia kura pendekezo la Marekani la kutaka kufanywe uchunguzi wa shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria.
Maafisa wa kibalozi wanasema hatua hiyo inaweza kusababisha mzozo na Urusi, ambayo inaweza kuamua kulipinga pendekezo hilo kwa kura ya turufu. Balozi wa Marekani Nikki Haley aliwaambia wanadiplomasia katika Baraza la Usalama kwamba Marekani inataka kuupigia kura mswada huo, ingawa Urusi inasema una mambo yasiyokubalika. "
Historia itaweka rekodi ya tukio hili kama wakati ambapo Baraza la Usalama limefanya kazi yake au limeshindwa kuwalinda watu wa Syria.Kwa njia yoyote ile Marekani itajibu," amesema Nikki Haley. Umoja wa Mataifa uliwasilisha rasimu ya mswada jana Jumatatu kufuatia madai ya kutumika gesi ya sumu katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Douma, shambulizi lililowauwa watu wapatao 40 na kumfanya Rais Donald Trump kuashiria kwamba huenda jeshi la Marekani likachukua hatua ya kijeshi, haraka.
alicho sema mchungaji philipo kuhusu kidada
Post a Comment