Header Ads

yaliyo jili tanzania kwanye michezo


Timu ya Taifa ya Vijana U-20 (Ngorongoro Heroes) wamepewa mapumziko ya siku tatu ili waweze kupumzisha miili yao ili waweze kujiweka sawa katika michezo inayokuja mbele yao.

Hayo yamewekwa bayana na Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) leo Aprili 24, 2018 baada ya wachezaji hao kuwasili nchini wakiwa wametokea nchini DR Congo kwenye mchezo  wake wa marudiano wa kufuzu fainali za Afrika za vijana U-20 dhidi ya DR Congo.
Ngorongoro Heroes katika raundi ya pili watacheza dhidi ya Mali mwezi ujao ambapo mchezo wao wa kwanza wakianzia katika dimba la nyumbani.

Serengeti Boys kuiangusha Kenya ?

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' kesho Aprili 25, 2018 wanatarajia kutupa karata yake nyingine muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Kenya nchini Burundi.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Afisa wa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari wa Jijini Dar es Salaam leo katika kuelekea mchezo huo.
Mchezo huo utachezwa majira ya saa 10:00 jioni kwenye dimba la Muyinga nchini Burundi.
Serengeti Boys walifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.
Kufuzu hatua ya nusu fainali Serengeti Boys walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kuifunga Sudan kwa magoli 6-0 kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B.
alieanza uchawi tangu mtoto mdogo aokoka
angalia hapa sylas tv

No comments