Header Ads

Marekani imefikia maamuzi kuhusu uwezekano wa kuyaondoa majeshi yake nchini Syria


Image result for Marekani imefikia maamuzi kuhusu uwezekano wa kuyaondoa majeshi


Marekani imefikia maamuzi kuhusu uwezekano wa kuyaondoa majeshi yake nchini Syria. Taarifa hii ni kulingana na afisa wa usalama wa ngazi ya juu wa Marekani aliyeongeza kuwa tangazo kuhusu hatua hiyo litatolewa hivi karibuni. 

Mkurugenzi wa usalama wa taifa Dan Coats amesema viongozi waandamizi wa serikali walikuwa miongoni mwa majadiliano muhimu kuhusu ahadi hiyo ya Marekani kuhusu Syria, yaliyofanyika ikulu ya White House hapo jana. 

Coats amesema taarifa itatolewa hivi karibuni kuhusu maamuzi yaliyofikiwa. Rais Donald Trump alisema hapo jana kwamba anataka wanajeshi wa Marekani kuondoka nchini Syria ingawa maafisa wa juu wa Marekani walisisitiza haja ya kubakia wanajeshi hao kwa kipindi kirefu. 

ALICHO KISEMA MCHUNGAJI SIKILIZA HAPA


No comments