Header Ads

Urusi yaishutumu Uingereza kuhusika na shambulizi la sumu

Image result for Vasily Nebenzya


Balozi wa Urusi kwenye Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya ameishutumu Uingereza kwa kuhusika na shambulizi la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi, Sergei Skripal pamoja na binti yake. Akilihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Nebenzya amesema idara ya ujasusi ya Uingereza huenda inahusika na kumpa sumu Skripal.

 Amesema Uingereza iliwahi kukiri kwamba ina sumu hiyo inayoathiri mishipa.

Amebainisha kuwa Urusi haina hati miliki ya sumu hiyo inayoitwa Novichok na kwamba ilitengenezwa kwenye nchi nyingi ikiwemo Uingereza na Marekani. Uingereza iliishutumu Urusi kwa kuhusika na shambulizi hilo la sumu lililotokea Machi 4 kwenye mji wa Salisbury. 

Hata hiyo, Urusi imekanusha madai hayo. Balozi wa Uingereza, Karen Pierce amesema nchi yake haitosikiliza maoni au ushauri kuhusu uwajibikaji wake, kutoka kwenye nchi ambayo mara kadhaa imezuia uchunguzi wa matumizi ya silaha za sumu nchini Syria.

ANGALIA HAPA CCM YA ZIDI KUTAMBA

No comments