Header Ads

CHADEMA waache kulia



Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Maulid Mtulia ametoa ushari kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ambacho ni Chama kikuu cha Upinzani kuwa waache kulia lia ila wagangamae (wakomae).
Mtulia ameyasema hayo jana alipokuwa akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019, mjini Dodoma
“Mh. Mwenyekiti mimi ni Mbunge nimeapishwa jana tu nimeingia kupitia dirisha dogo na mara nyingi wachezaji wanaoingia kupitia dirisha dogo ni wachezaji wazuri sana nikishukuru chama changu Chama cha Mapinduzi kwa kunipa fursa hii adhimu kabisa hatimae kuwagalagaza jamaa zetu kule na kupata ushindi wa kishindo ni mshukuru Rais wangu, Dkt John Pombe Magufuli mimi namuita Field Masha na niliwaambia nampenda balaa nampenda kweli kweli kwa namna anavyochapa kazi  nitakuwa sijafanya sawa nisipo mshukuru Makamu wa Rais Mama Samia kwa namna anavyomsaidia Rais wetu katika kutekeleza majukumu yetu,”
“Ushauri kwa chama changu kile kilichonilea kwamba kibaya kwako chema kina wenyewe lakini ushauri wangu kwa Chama kikuu cha Upinzani (Chadema) waache kulia kulia wagangamale kulonda kazi ya Jeshi kugangamala kama umeingia kwenye uchaguzi umepigwa unafanya tathmini unajipanga kwaajili ya uchaguzi ujao, mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine  tuonane 2020 na Inshallah Maulid Mtulia mtamkuta palepale Kinondoni

No comments