Klabu ya soka ya Manchester United imetinga hatua ya fainali ya Kombe kongwe zaidi duniani
Tottenham ndio walikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 11 kupitia kwa kiungo Delle Alli kabla ya mshambuliaji Alexis Sanchez kusawazisha bao hilo dakika ya 24 na kufanya kipindi cha kwanza kimalizike kwa sare.
Kipindi cha pili Manchester United walijihakikishia kucheza fainali baada ya kiungo wa Kihispania Ander Herrera kufunga bao la pili dakika ya 62 na kuzima ndoto za Tottenham za kusaka walau taji moja baada ya kuwa na kikosi bora kwa misimu kadhaa.
Man United sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Chelsea inayofundishwa na Conte ambayo itacheza na Southampton inayofundishwa na Mark Hughes. Nusu fainali hiyo itapigwa kesho kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
simba fc kujitapa
Post a Comment