Julius Maada Bio ameapishwa kuwa rais mpya wa nchi Sierra
Mgombea wa upinzani nchini Sierra Leone ambaye zamani alikuwa kiongozi wa kijeshi Julius Maada Bio ameapishwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo saa chache tu baada ya tume ya uchaguzi kutangaza ushindi wake katika kinyang’anyiro kilichokuwa na ushindani mkali.
Bio alimshinda mgombea wa chama kinachotawala cha All People’s Congress, Samura Kamara kwa kupata asilimia 51.81.
Kamara amevieleza vyombo vya habari kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu na kwamba anapanga kuchukua hatua za kisheria.
chama cha mapinduzi ccm mkoa wa tabora angalia hapa
Post a Comment