Rais Magufuli ameyasema hao leo alipokuwa akizindua kituo cha kuzalisha umeme
Rais Magufuli ameyasema hao leo alipokuwa akizindua kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II, ambapo amesema kwamba kwa sasa miradi yote ya umeme ukijumlisha na wa Stiegler Gauge itafikia megawati 5000 , hivyo ni wakati muafaka wa wizara husika kufikiria namna ya kupunguza bei ya umeme.
“Muanze kufikiria namna ya kushusha bei ya umeme, mmeanza vizuri muendelee na utaratibu huo. “Nchi ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme, maji , jua, upepo, makaa ya mawe, hata nyuklia, kwa sababu tunayo madini ya uranium yanayoweza kuzalisha umeme kwa nyuklia, kwa umeme wote huo hakuna haja ya kuwa na bei ya juu, ”amesema Magufuli.
Rais Magufuli ameendela kwa kusema kwamba nchi itakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na kwa gharama nafuu, kwani hapo awali umeme ulikuwa ghali kutokana na umeme mwingi kuzalishwa kwa kutumia mafuta (dizeli).
Post a Comment