Header Ads

Yanga ya PEWA uwanja


Klabu ya Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imefunguka na kudai wamekabidhiwa kiwanja chenye takribani hekari 50 Mkoa Dodoma kwa lengo la ujenzi wa 'academy' itakayokuwa inakuza vipaji vya vijana wadogo nchini Tanzania.


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na uongozi huo kupitia ukurasa wao maalum wa kijamii asubuhi ya baada ya kumaliza shughuli za ufunguzi wa tawi la jipya la Yanga katika makao makuu ya nchi, mkoani Dodoma.  
"Wanachama wa Yanga tawi la Dodoma Makao Makuu kupitia mlezi, Naibu waziri wa kazi, vijana na Ajira , Antony Mavunde, wametoa eneo la hekari 50 kwa Yanga SC kwa ajili ya ujenzi wa 'academy' ya klabu itakayokuwa na jukumu la kutafuta, kukuza na kendeleza vipaji kwa vijana wadogo ili waje kuwa wachezaji wakubwa wa Yanga katika siku za usoni", imesema taarifa hiyo.
Picha ya wanachama wa Yanga baada ya ufunguzi wa tawi lao jipya huko Dodoma.
Kwa upande mwingine, matumaini ya Yanga SC kutetea ubingwa wake wa Ligi kuu Tanzania Bara yamezidi kuonekana kuwa hafifu baada ya jana Aprili 22, 2018 kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Mbeya City uwanja wa Sokoine na kusababisha kuwa na alama 48 katika mechi 23 huku wakiwa wamezidiwa alama 11 na watani wao wa jadi Simba SC wenye pointi 59 za mechi 25 na wababe hao watakutana Jumapili uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
.
SIKIA ALICHO SEMA MSUKUMA

No comments