Header Ads

KOCHA Mkuu wa timu ya Majimaji FC ya Songea mkoani Ruvuma, Peter Mhina ameahidi ushindi


Image result for majimaji fc



KOCHA Mkuu wa timu ya Majimaji FC ya Songea mkoani Ruvuma, Peter Mhina ameahidi ushindi kuelekea mchezo wake wa wikiendi hii dhidi ya Ruvu Shooting katika Uwanja wa CCM mjini Songea.
Akizungumza na gazeti hili, Mhina alisema timu yake imekuwa ikijiandaa vyema na mchezo huo tokea irejee kutoka mkoani Mwanza ilipocheza na Mbao FC na kutoka sare ya 2-2.
Alisema wamefanya mazoezi vya kutosha, ambapo katika mazoezi hayo alisema wamefanikiwa kurekebisha makosa yao yaliopelekea kupata sare dhidi ya Mbao FC.
Mhina alisema amewajenga vyema vijana wake kisaikolojia ili kuhakikisha wanapambana na kushinda dhidi ya Ruvu Shooting.
Alisema ana imani kubwa sana na timu yake itapambana na kuweza kuibuka na ushindi.
Mchezaji huyo wa zamani wa timu za African Sports na Maji Maji FC alisema atahakikisha wanashinda na mechi zao zote zilizobakia dhidi ya Azam FC, Singida United, Mtibwa Sugar na Simba SC.
Katika msimamo wa Ligi Kuu, Majimaji ina alama 20 ipo katika nafasi ya 15. Timu hiyo imeshinda mechi 3, sare 11 na kupoteza mechi 11.

No comments