Header Ads

uhuru wa habari duniani unakabiliwa na vitisho


Image result for Shirika la Maripota wasio na mipaka limesema uhuru wa habari duniani


Shirika la Maripota wasio na mipaka limesema uhuru wa habari duniani unakabiliwa na vitisho vitatu vya juhudi za Rais wa Marekani Donald Trump, Urusi na China kuzima upinzani. 

Shirika hilo linalojulikana kwa kifupi kama RSF, limeonya kuwa mazingira ya chuki na uhasama kwa waandishi habari, ikijumlishwa na juhudi zinazozidi za kudhibiti vyombo vya habari vinatoa kitisho kwa demokrasia. 

Katika ripoti yake ya kila mwaka, RSF imesema waandishi habari walilengwa katika wimbi kubwa na utawala wa mkono wa chuma ambapo viongozi wamekuwa wakichochea chuki dhidi yao. Shirika hilo limeyatuhumu mataifa makubwa matatu duniani 
Marekani, Urusi na China - kwa kuongoza ukandamizaji dhidi ya uhuru wa habari, ambapo Trump amekuwa akianzisha mashambulizi binafsi ya mara kwa mara dhidi ya waandishi, na serikali mjini Beijing ikishutumiwa kuhamisha ruwaza yake ya udhibiti wa vyombo vya habari kuminya upinzani kwingineko barani Asia.


chanzo dw swahili

No comments