Header Ads

Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania imetoa muda wa mwisho wa wiki mbili kwa wamiliki wa blogger


Image result for blogu



Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania imetoa muda wa mwisho wa wiki mbili kwa wamiliki wa blogger kuandikisha mitandao yao chini ya sheria kali za maudhui ya mitandao ya kijamii, 

huku kukiwa na wasi wasi kwamba serikali inabana uhuru wa watumiaji wa mtandao wa intaneti. Sheria iliyopitishwa mwezi Machi inafanya kuwa lazima kwa wenye blogu na wamiliki wa majukwaa ya mtandaoni kama televisheni za mtandao wa Youtube kujiandikisha katika serikali na kulipa kiasi cha dola 900 sawa na zaidi ya shilingi za Tanzania milioni 2 ili kupata leseni.

 Wanaharakati wa kidijitali wanasema hatua hiyo ni sehemu nyengine ya ukandamizaji wa serikali dhidi ya upinzani na uhuru wa kutoa maoni unaofanywa na serikali ya Rais John Pombe Magufuli, ambaye alichaguliwa mwaka 2015 na kuahidi kuharakisha ukuaji wa uchumi na maendeleo. 

Waombaji wanatakiwa kutoa maelezo ya wadau, mtaji, uraia wa mmiliki, ujuzi wa wafanyakazi na mipango ya mafunzo, pamoja na hati ya malipo ya kodi.

chanzo dw kiswahili

 wasukuma watoa mpya angalia sylas denniss tv
hapa chini


No comments