Yanga yatangaza mbinu zake za kuikarisha Simba
Yakiwa yamebakia masaa kadhaa kuelekea katika mtanange wa kukata na shoka 'Kariakoo derby', klabu ya Yanga imeibuka na kudai hawana shaka yeyote kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Simba kwani wao wanachosubiri ni dakika 90 za uwanjani nasio kitu kingine.
Hayo yamebainisha na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Dismas Ten na kusema kuwa maandaalizi ya mechi hiyo yamekamilika kwa asilimia 100.
"Mazoezi ya siku nane yamefanyika kwa umakini mkubwa kwa upande wa timu na kwa upande wa uongozi maanadalizi yote muhimu yamekwisha fanyika na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za uwanjani. Hali ya wachezaji ipo vizuri kabisa kasoro Ngoma pekee bado yuko nje ya kikosi kwa majeraha. Suala la nani ataanza au kutocheza tumewaachia benchi la ufundi kuona nani wanaweza kumtumia kulingana na ‘game plan’ waliyokuwa nayo", amesema Dismas.
Katika hatua nyingine Kocha Zahera Mwinyi amesema ameridhishwa na uwezo wa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha Yanga,anachohitaji ni muda wa kukaa nao ili aendelee kuwajenga na kuwaimarisha zaidi tayari kwa michezo ya kimataifa.
makonda na msukuma ulingoni
angalia hapa chini
Post a Comment