Amuuwa mpenzi wake kwa kumnyonga
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia kijana aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) mkazi wa Mtaa wa Mahama Ilemela kwa kunyonga mpenzi wake Victoria Swai (26).
Inadaiwa kijana huyo alifanya mauaji hayo kwa kumkaba shingo mpenzi wake huyo hali iliyopelekea kukosa hewa na baadae kufariki dunia.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kudai tukio hilo limetokea katika jengo la Ekacliff ofisi ya Kilimanjaro Avitaion.
Katika tukio hilo polisi walifanya uchunguzi katika nyumba alipokuwa akiishi marehemu na mpenzi wake na kumkuta mtuhumiwa akiwa amejificha juu ya dari ya nyumba.
Chanzo cha mauaji hayo kinadaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa alikuwa akimsaliti kimapenzi ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
Post a Comment