Tanzania yaomba ufadhili wa mradi tiegler Gorge kutoka AfDB
Tanzania imeiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kufadhili mradi wake wa kuzalisha umeme wa maji wa megawati 2,100 katika maporomoko ya Mto Rufiji.
Taifa hilo la Afrika Mashariki linauangalia mradi huo wa Stiegler Gorge katika Hifadhi ya Mbuga ya Selous inayotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Utamaduni (UNESCO) kama urithi wa dunia kuwa muhimu katika kukomesha tatizo sugu la uhaba wa umeme nchini humo. Wizara ya Fedha ya Tanzania imesema katika taarifa yake ya jana Jumamosi kwamba Rais John Magufuli,
ambaye anahusika moja kwa moja katika mradi huo uliozorota kwa muda mrefu, aliwasilisha ombi hilo la fedha kwa Rais Akinwumi Adesina wa Benki ya AfDB wakati wa mazungumzo nchini Tanzania katika mji mkuu wa Dodoma
mwishoni mwa wiki. AfDB imethibitisha kwamba imelipitia
ombi la Magufuli lakini halikutaja gharama za mradi huo. Lakini wakosoaji wanasema kupata ufadhili wa mradi huo itakuwa vigumu kwa sababu ujenzi wa bwawa la maji katika mto unaopita katika hifadhi ya Selous utaathiri wanyama pori na makaazi yao.
AIBU YA KUMBA NANDI ANGALIA SYLAS TV
hapachini
Post a Comment