Mbeya City imeanza safari yake leo kuelekea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo huo wa ligi kuu
Timu ya Mbeya City itawakosa nyota wake wakutumainiwa ambao ni walinzi John
Kabanda na
Hassan Mwasapili, kwenye mchezo wake wa Ligi Kuu ya dhidi ya Simba SC utakaopigwa
Alhamisi hii.
Mbeya City imeanza safari yake leo kuelekea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo huo wa ligi kuu raundi ya 24, lakini inakabiliwa na pigo hilo la kuwakosa mabeki wake hao wa kati kwa matatizo mawili tofauti.
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Mrundi Ramadhani Nswanzurimo amesema kuwa Mwasapili ataukosa mchezo huo kwasababu anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano huku John Kabanda akiwa nje kutokana na kuwa majeruhi.
Azam FC itaingia kwenye mchezo dhidi ya Simba ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare nyumbani dhidi ya Azam FC jumapili iliyopita. Simba nayo imetoka kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jana April 9.
burudani kutoka tabora
Post a Comment