Wanajihadi waua zaidi ya watu 30
Zaidi ya watu 30 wa kabila la Tuareg wameuliwa na wapiganaji wa kijihadi nchini Mali katika eneo la kaskazini-mashariki linalopakana na Niger.
Kundi la zamani la waasi wa Tuareg la MSA pamoja na viongozi wa makabila wamesema, shambulio hilo limetokea siku moja baada ya washambuliaji waliokuwa katika pikipiki kuwauwa watu 12 karibu na eneo la Anderamboukane.
Katika wiki za hivi karibuni, kumezuka vurugu upya katika taifa hilo la Afrika. Mapema mwezi huu, kambi ya Umoja wa Mataifa katika mji wa Timbuktu ilishambuliwa kwa mabomu ya roketi na mabomu yaliyotegwa ndani ya magari, na kuua askari mmoja wa kulinda amani na kujeruhi wengine saba. Umoja wa Mataifa umeonya mwezi uliopita kwamba usalama unazidi kuzorota nchini Mali, na vurugu zinasambaa hadi nchi jirani.
msukuma na makonda ulingoni
angalia video sylas denniss
Post a Comment