Kifo cha msanii wa bongo fleva Jebby ambaye amefariki jana April 22, 2018
Kifo cha msanii wa bongo fleva Jebby ambaye amefariki jana April 22, 2018 kwa matatizo ya bandama akiwa mjini Dodoma kimenifanya kutafakari na kurudi nyuma na kuwakumbuka ndugu zetu wengine katika sanaa ambao wametangulia mbele za haki na kutuachia kumbukumbu ya kazi zao ambazo zinadumu.
Mara zote inapotokea taarifa ya kifo hasa cha watu maarufu ambao tumewafahamu kupitia kazi zao huwa taarifa zao zinawagusa watu na kuwaumiza pia lakini kwa namna moja au nyingine kupitia vifi vyao huwa tunakumbushwa mambo ya msingi kama binadamu.
Bila kupepesa macho ni wazi kuwa vifo vya wasanii wafuatao vimeacha pengo kubwa katika tasnia ya muziki wa bongo fleva kutokana na ukweli kwamba ni watu ambao walikuwa wakifanya muziki wa bongo fleva kwa namna ya pekee, walileta changamoto mbalimbali kwenye sanaa na kuifanya tasnia hiyo kupiga hatua kwa namna moja au nyingine ndiyo maana hata sasa ukitazama na kusikiliza kazi zao utagundua kuwa nafasi zao hazijaweza kuzibwa kutokana na upekee wa wasanii hao katika kazi zao na mchango wao kwenye tasnia.
Mei 28, 2013 msanii maarufu wa Hip Hop nchini, Albert Mangwair (Mangwea) alifariki dunia nchini Afrika Kusini katika hospitali ya Helen Joseph ya jijini Johanesburg ni wazi kuwa Mangwea ataendelea kukubwa kutokana na kazi zake nyingi kali alizoziacha hivyo ameacha alama kubwa katika muziki wa bongo fleva.
Desemba 2, 2011 msaniii wa muziki wa kizazi kipya, Abeli Motika alimaarufu kwa jina la Mr .Ebbo alifariki dunia, Mr. Ebbo aliibuka vyema na staili yake ya kuimba kama Masai na kuweza kukonga nyonyo za watu wengi, kupitia staili yake hiyo aliweza kuimba vitu ambavyo vilikuwa vikiwachekesha watu kupitia muziki wake hivyo amekuwa na mchango mkubwa sana katika muziki wa bongo fleva.
Juni 13, 2013 msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Langa Mengisen Kileo, alifariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, Langa ni kati ya watu ambao alileta chachu kwenye muziki wa rap bongo, mkali huyu aliibuka kwenye mashindano ya Coca-Cola pop star mwaka 2003 na baadae waliunda kundi lililowajumuisha Witness and Shaa kundi hilo lilifahamika kama Wakilisha.
Novemba 27, 2012 msanii/muigizaji/mchekeshaji Hussein Ramadhani Mtioeti aliyekuwa maarufu kama Sharo Milione alifariki dunia katika ajali ya gari jijini Tanga. Shoro Milionea alifanya muziki wa bongo fleva lakini muziki wake pia ulikuwa na lengo la kufurahisha na kuburudisha tu.
Mei 17, 2017 msanii wa bongo fleva, Mfaume Selemani 'Dogo Mfaume', aliyetamba zaidi na wimbo wake wa Kazi ya dukani alifariki dunia, Dogo Mfaume ni kati ya watu wachache ambao walikuwa wakifanya muziki wa bongo fleva kwa maazi ya Mchiriku/ Mnanda.
Januari 8, 2013 Msanii nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, alifariki, Omari Omari alileta mapinduzi kwenye muziki wa bongo fleva kwa wasanii ambao walikuwa wakiimba Mchiriku kwani kazi zake ziliweza kufanya vizuri na kutamba karibu kila kona, hivyo alileta chachu katika muziki wa bongo fleva na kuupa nguvu muziki huo hasa zaidi kwa wasanii ambao walikuwa wakiimba Mchiriku na Mnanda.
Steve 2 K alitamba na kundi la Mambo poa msanii huyu aliuawa kwa kuchomwa kisu na producer Castol mwaka 2004 na chanzo cha kuchomwa kisu kilielezwa ni kutofautiana na mtayarishaji huyo.
Agosti 21, 2015 Vivian na Complex walifariki dunia kwa ajali ya gari ambayo ilitokea eneo la Mbwembwe Tanga na kukatisha maisha yao, wasanii hawa wawili walikuwa ni wapenzi.
Februari 20, 2015 msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Chamber Squad, Moses Frank Mshangama maarufu kwa jina la 'Mez B' alifariki dunia akiwa mjini Dodoma
Oktoba 21, 2014 msanii wa muziki YP alifariki dunia baada ya kusumbuliwa na tatizo la kifua ambalo alikuwa nalo kwa muda mrefu. Msani huyo alikuwa ni mmoja kati ya wasanii ambao walikuwa wakiunda kundi la Wanaume TMK Family.
Machi 29, 2006 Father Nelly alifariki dunia kwa kuchomwa kisu jijini Arusha ambapo alikuwa anakwenda kuamua ugomvi wa watu wawili ambao walikuwa wakigombana, Father Nelly ni mmoja wa watu walioanza kurap mapema zaidi huko Arusha kuanzia mwaka 1992/93 akiwa na umri mdogo kabisa na kuhamasisha vijana wengi kuingia katika muziki huo wa rap, hivyo mchango wake katika muziki ni mkubwa sana.
Agosti 27, 2002 Cool James alimaarufu kama Mtoto wa Dandu alifariki dunia kwa ajali ya gari, licha ya kufanya mapinduzi makubwa ya muziki wa bongo fleva lakini pia msanii huyo ndiye muasisi wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards ambazo awali zilikuwa zikifahamika kama Tanzania Music Awards (TAMA)
Machi 21, 2011 muimbaji maarufu wa nyimbo za taarabu Issa Kijito alifariki dunia kwa ajali ya gari katika maeneo ya Mikumi, Morogoro katika ajali hiyo wasanii wengine 12 wa kundi la muziki wa Taarab za 5 Star pia walipoteza maisha.
Februari 12, 2008 msanii wa muziki wa kizazi kipya, John Mjema 'Bomba la Mvua' alifariki dunia baada ya kujichoma kisu mwenyewe sehemu ya shingo
April 17, 2013 msanii maarufu visiwani Zanzibar, Afrika Mashariki na nje ya bara hilo Fatuma Bint Mbaraka maarufu kwa jina la Bi Kidude, alifariki dunia, Bi Kidude alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 103 na katika kipindi cha uhai wake alifanya mambo mengi sana katika muziki hususani muziki wa taarabu.
Post a Comment