UFAHAMA UNGONJWA WA Kisonono (gonorrhea) ni nini?
Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina
ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka katika
sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa
wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na
kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi
(cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka
15-19 wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri
wa miaka 20 -wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Ugonjwa
huu huambukizwa vipi?
Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja
kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye
sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum). Ugonjwa wa gono
huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi
mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya kulevya.Dalili za ugonjwa wa kisonono
Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7
baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili ni kama
zifuatazo;
Kwa
wanaume:
- Kuhisi kama kichomi wakati wa
kukojoa (burning sensation)
- Kutokwa na majimaji ya njano au
meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali
sana
- Wakati mwengine maumivu au
kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
- Maambukizi yakiwa kwenye puru
(rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa
sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na
damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.
Kwa wanawake:
- Dalili kwa wanawake huwa si
nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote
- Maumivu au kuhisi kama kichomi
wakati wa kukojoa
- Kuongezeka kwa kutoka majimaji
kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na
damu
- Kutokwa na damu kupitia tupu ya
mwanamke kabla ya hedhi kufika.
- Kutokwa na damu baada ya
kujamiana au baada ya tendo la ndoa
- Kichefuchefu
- Homa (fever)
- Kutapika
Vipimo vya ugonjwa wa
kisonono
- Swab for culture Kipimo hiki
hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri
kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono.
- Polymerase Chain Reaction (PCR)
Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.
Tiba ya ugonjwa wa
kisonono ni nini?
Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi
magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama
mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya
kizazi (cervix), urethra na
puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za
aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin
(mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa wale chini
ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano. Fuata
ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi kwani dawa nyingi zina madhara
kwa wajawazito (mfano doxycyclin). Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote
wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za
ugonjwa huu.Madhara ya ugonjwa wa kisonono
- Kutoweza kuzaa kwa mwanamke
(tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
- Huweza kuathiri moyo (heart
valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
- Madhara kwenye sehemu za maungio
au jointi (joint inflammation)
- Kwa wanawake wale ambao
hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease)
ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
- Wale wanawake ambao ni
wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au
kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor).
- Kwa wale wanaoambukizwa gono
kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na
hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu (blindness),
homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).
Kinga ya
kisonono
- Kutumia kondomu wakati wa
kujamiana
- Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
- Kuacha vitendo vya ngono kama
matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
- Kwa wanawake wajawazito
Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa
tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwengine
wowote.
- Wanawake wajawazito
wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto ameathirika na gono
apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha kuwa kipofu.
- Epuka kufanya ngono na mtu
aliyeambukizwa gono.
"Kumbuka ya kwamba hakuna kitu kama ngono salama kwani huwezi kujua kama
wewe au mwenzako wakati wa kujamiana ameathirika au la, au una michibuko au
umekatika kwenye ngozi au la kwani michibuko mengine inaweza isionekane au
kugundulika kwa urahisi. Njia pekee na nzuri ni kuacha au kujikinga na vitendo
vya ngono". Mtu aliyepata gono awali anaweza kupata tena.
ummu kulthum Aende hospitali kupiga Sindano haraka iwezekanavyo
MSUKUMA NA PENDO PENEZA WAKATAANA
Post a Comment