Header Ads

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anausitisha mkataba na Umoja wa Mataifa UN


Image result for Israel Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema anausitisha mkataba na Umoja wa Mataifa wa kuwapeleka katika nchi za magharibi wahamiaji 16,000 wa Kiafrika wanaotafuta hifadhi, katika nchi za Magharibi.

 Netanyahu ameubadili msimamo wake saa chache tu baada ya kutangaza makubaliano hayo. Kwenye taarifa katika ukurasa wake wa Facebook, Netanyahu amesema atajadiliana kwanza na wakaazi wa kusini mwa Tel Aviv, kabla ya kuudurusu tena mkataba huo utakaowaruhusu wahamiaji wengine 16, 000 kupewa hifadhi rasmi nchini Israel. 

Kabla ya kuubadili msimamo wake, Netanyahu alisema makubaliano hayo ni mazuri na utawawezesha kutatua tatizo kwa njia inayofaa na inayoyalinda masilahi ya Israel na wakaazi wa kusini mwa Tel Aviv na majirani wengine. 

Mkataba huo ambao Netanyahu aliutangaza jana jioni, ungesitisha mpango wa Israel kuwarudisha maelfu ya wahamiaji wa kiafrika katika nchi zao, na pia ungemaliza mwongo mmoja wa wahamiaji hao kutojua hatima yao. Kulingana na takwimu za serikali ya Israel, kuna takriban wahamiaji 37,000 na maelfu ya watoto wanaotafuta hifadhi nchini humo.

CHANZO DW KISWAHILI


uwezo wa jwt tanzama hapa

No comments