kambi ya kijeshi ya Syria imeshambuliwa
Vyombo vya habari vya serikali ya Syria vimeripoti kuwa kambi ya kijeshi nchini humo imeshambuliwa kwa makombora huku Marekani na Ufaransa zikikanusha kuhusika na mashambulizi.
Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron waliapa kuchukua hatua kali dhidi ya utawala wa Syria baada ya majeshi ya nchi hiyo kudaiwa kufanya shambulizi la silaha za sumu dhidi ya raia mjini Douma.Serikali ya Ujerumani imelaani shambulizi hilo pia, ikisema Urusi kama mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inawajibika,
na kuongeza kuwa utawala wa Syria haungeweza kufanya mashambulizi kama hayo bila ya usaidizi kutoka kwa Urusi na Iran.Shambulizi hilo la sumu limelaaniwa vikali na jumuiya ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya kikao cha dharura leo kulijadili. Syria imeripoti kuwa makombora kadhaa yameshambulia kambi ya jeshi iliyoko katika jimbo la Homs.Syria na Urusi zimeishutumu Israel kwa kufanya mashambulizi hayo yaliyowaua wanajeshi 14 wa Syria na washirika wake.
MARUFUNGU ASKALI KUKATA BANGI
Post a Comment