Header Ads

Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amewasili katika jela la Curibita kuanza kutumikia kifungo cha miaka 12



Image result for Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio


Rais wa zamani wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva amewasili katika jela la Curibita kuanza kutumikia kifungo cha miaka 12 jela baada ya siku ya Ijumaa, mahakama kumhukumu kwa mashitaka ya ufisadi. 

Matangazo ya moja kwa moja ya vituo vya televisheni vya Brazil yameonesha akiwasili kwa helikopta katika makao makuu ya polisi katika mji wa Curibita ulioko kusini mwa Brazil. Hayo yanakuja baada ya Lula da Silva kujisalimisha kwa polisi. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 72 aliondoka Sao Paoli akiwa amezingirwa na walinzi kwenye jengo la muungano wa wafuaji vyuma mjini humo.

Alipenya katikati ya wafuasi wake waliokuwa wanamzuia asiondoke na kuingia katika gari la polisi. Anasisitiza kuwa mashitaka dhidi yake yalichochewa kisiasa.

 Lula alikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka kwenye kampuni kubwa ya ujenzi, ili iweze kupata mikataba ya serikali.

No comments