Rais wazamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kufikishwa mahakamni hapo kesho Ijumaa akikabiliwa na mashitaka 16
Rais wazamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kufikishwa mahakamni hapo kesho Ijumaa akikabiliwa na mashitaka 16 yanayohusishwa na mkataba wa mauzo ya silaha, kashfa iliyomuandama wakati wa utawala wake kabla ya kuondolewa madarakani Februri mwaka huu.
Zuma atafika katika mahakama kuu ya mjini Durban iliyoko kwenye jimbo lake la nyumbani la KwaZulu-Natal kwa ajili ya hatua ya awali ya shauri hilo katika kesi ambayo inaweza kumpeleka gerezani. Makundi ya wafuasi wa Zuma pamoja na wapinzani wake kisiasa wanatarajiwa kuandamana nje ya mahakama
ambako kunatarajiwa kuwepo idadi kubwa ya maafisa wa polisi kwa ajili ya kuzuia vurugu. Zuma anatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kampuni ya kutengeneza silaha ya Ufaransa ya Thales kuhusiana na kandarasi ya thamani ya dola bilioni 5 wakati alipokuwa waziri wa uchumi na pia naibu rais wa chama cha ANC.
SIRI YA UCHAWI ANGALIA HAPA SYLAS TV
Post a Comment