matokeo yote ya michezo ya kimataifa
Eliud Kipchoge wa Kenya ameshinda mbio ndefu za London Marathon kwa mara ya tatu. Alishinda katika mwaka wa 2015 na 2016
Bingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge ameshinda taji lake la tatu la mbio ndefu marathon mjini London jana Jumapili na kukamilisha ushindi mara mbili wa Wakenya baada ya Vivian Cheruiyot kushinda mbio hizo kwa upande wa wanawake.
Kipchoge mwenye umri wa miaka 33, alimshinda Muithiopia Tola Shura pamoja na Mo Farah wa Uingereza na kushinda mbio zake za tatu za London Marathon kwa kutumia muda wa masaa 2 dakika 4 na sekunde 17, akimaliza zaidi ya nusu dakika mbele ya Kitata na Mo Farah akiwa wa tatu kwa kutumia masaa 2 dakika 21 na sekunde 40.
Bayern Munich yaisubiri Real Madrid
Bayern yaisubiri kwa hamu Real Madrid katika mtanange wa Champions League wa kulipiza kisasi.
Champions League inarejea uwanjani tena kesho na keshokutwa Jumatano katika awamu ya nusu fainali, ambapo klabu kutoka ligi nne kubwa za Ulaya zinawakilishwa. Kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1981, timu kutoka Uhispania , Real Madrid England Liverpool, Italia Roma na Ujerumani Bayern Munich zinakuwa timu nne za mwisho katika kinyang'anyiro hicho cha juu cha vilabu barani Ulaya.
FC Kolon yachungulia daraja la pili
Hakuna jicho lililokosa machozi jana mjini Kolon wakati FC Kolon ilipotumbukia katika shimo la kushuka daraja ... wakati Hamburg SV yapata matumaini kwa mbali ya kubakia katika Bundesliga.
Schalke 04 imeweka mguu mmoja katika michuano ya Champions League msimu ujao wakati FC Kolon iko katika ukingo wa kushuka daraja baada ya sare ya mabo 2-2 jana Jumapili. Wachezaji pamoja na mashabiki wa FC Kolon macho yalimiminika machozi kuiona timu yao ikiporomoja licha ya kufanya juhudi za ziada kwa kupata ushindi muhimu jana.
Kolon walihitaji kupata ushindi jana ili kuweka hai matumaini yao ya kubakia katika daraja la kwanza lakini mabao ya haraka haraka mnamo kipindi cha kwanza ya Breel Embolo na Yevhen Konoplyanka yakiwakatisha tamaa , licha ya kupigana kufa na kupona na kukomboa mabao hayoMarcel Risse ndie aliyefunga bao la kukomboa la FC Kolon jana.
Arsene Wenger kuachia ngazi mwishoni mwa msimu
Makocha wa timu za ligi kuu ya England Premier League pamoja na wachezaji wa zamani wamemmiminia sifa kocha wa Arsenal London Arene Wenger Ijumaa (20.04.2018) baada ya kutangaza atajiuzulu kuifunza timu hiyo.
Wenger mwenye umri wa miaka 68 alishinda mataji matatu ya Premier League na vikombe saba vya kombe la FA katika kipindi cha miaka 22 akiwa katika uongozi wa timu ya Arsenal lakini misimu ya hivi karibuni imeamsha hali ya kutoridhika miongoni mwa mashabiki wakati klabu hiyo ilishindwa kupambana kuwania taji la ligi
Schalke yawika mbele ya Dortmund
Ulikuwa mtanange uliosubiriwa na wengi mwishoni mwa wiki na sio tu kwa sababu ya utani wa tangu jadi wa timu hizo mbili, bali pia katika harakati za kutafuta nafasi ya Champions League. Schalke ikaizaba BVB 2-0
Schalke waliwazaba Borussia Dortmund mabao mawili na kujiimarisha katika nafasi ya pili ya msimamo wa Bundesliga. Hiyo bila shaka na hatua kubwa katika matumaini ya kupata tikiti ya moja kwa moja ya kucheza Champions League. Ushindi huo uliwapa nafasi ya kupumua kidogo maana sasa wana pengo la pointi nane kati yao na nambari tano RB Leipzig huku zikisalia mechi nne msimu kukamilika
kichapo hicho cha kwanza cha derby kwa Dprtmund tangu Septemba 2014 kimeiteremsha timu hiyo katika nafasi ya nne, nyuma ya Bayer Leverkusen na tofauti ya mabao. BVB iko nyuma ya Schalke na pengo la pointi nne na nne mbele ya Leipzig ambao walitoka sare ya bao moja kwa moja na Werder Bremen katika mechi nyingine ya jana.
Bayern mabingwa tena Bundesliga
Bayern Munich yanyakua rasmi ubingwa wake wa sita mfululizo katika Bundesliga , Borussia Dortmund yajisahihisha na kuimarisha nafasi yake ya kucheza Ulaya.
Bayern Munich imetia kibindoni taji lake la 28 la Bundesliga wiki hii baada ya kutawazwa tena kwa mara ya sita mfululizo kuwa mabingwa siku ya Jumamosi baada ya kuikandika Augsburg kwa mabao 4-1. Bayern imedhihirisha kwamba wao ni washindi wasioshindia katika Bundesliga.
F1: Ricciardo aibuka mshindi nchini China
Katika mashindano ya magari ya Formula One, dereva Daniel Ricciardo wa timu ya Red Bull aliibuka mshindi wa mashindano ya Grand Prix ya China, ikiwa ni wa sita katika taaluma yake ya mashindano hayo
Muasutralia huyo alichukua usukani katika mzunguko wa 45 baada ya kumpiku dereva wa Mercedes Valtteri Bottas. Bottas alimaliza katika nafasi ya pili huku Kimi Raikkonen wa Ferrari akipanda jukwaani katika nafasi ya tatu.
Mjerumani Sebastian Vettel ambaye ameshinda mikondo miwili ya kwanza msimu huu, alimaliza katika nafasi ya nane baada ya kuanza mashindano hayo akiwa katika nafasi ya kwanza. Pia aligongana na dereva wa Red Bull Max Verstappen na hivyo akapoteza nafasi kadhaa. Vettel bado anaongoza msimamo wa ubingwa wa dunia msimu huu akiwa na pointi 54, baada ya mikondo mitatu.
Lewis Hamilton, bingwa mara nne wa dunia na ambaye anatetea taji hilo, alimaliza katika nafasi ya nne na mpaka sasa ana pointi 43. Bottas ana pointi 40 katika nafasi ya tatu kabla ya mkondo ujao wa Azerbaijan.
Manchester City wabeba ubingwa wa England
Nchini England, Manchester City walitangazwa jana kuwa washindi wa Premier League baada ya nambari mbili Manchester United kuduwazwa katika uwanja wa nyumbani na Westbromwich Albion bao 1 -0.
Wiki moja baada ya City kuzabwa 3-2 na United na kupoteza nafasi ya kutwaa ubingwa dhidi ya mahasimu hao wakali, ni West Brom inayochungulia kaburi la kushushwa ngazi ambayo iliwasaidia City kuanza sherehe za mapema za kunyakua taji hilo rasmi.
Ligue 1
Na nchini Ufaransa, Paris Saint Germain imejiunga na Manchester City ya England na Bayern Munich ya Ujerumani katika sherehe za ubingwa wa ligi. PSG walinyakuwa taji la Ufaransa jana kwa kuwazaba mabingwa watetezi Monaco mabao 7-1. Ushindi huo mkubwa ulidhihirisha pengo kubwa lilipo kati ya timu hizo mbili msimu huu. Ni taji la tano la tano al PSG katika misimu sita na la saba kwa jumla. PSG wako mbele ya nambari mbili Monaco kwa pengo la pointi 17 wakati kukiwa na mechi tano zilizosalia msimu huu.
Charlie nani? Mwendesha baiskeli mwanafunzi ashinda dhahabu Madola
Si hata mashabiki wa mbio za baiskeli waliwahi kumsikia Charlie Tanfield mwaka mmoja uliopita, lakini sasa Mwingereza huyo kijana ni bingwa wa michezo ya Jumuiya ya Madola, akiweka rekodi ya muda mrefu.
Charlie Tanfield akisherehekea baada ya ushindi katika mbio za mwendeshaji mmoja mmoja za mita 4000 huko Anna Meares velodrome - Gold Coast, Australia, Aprili 6, 2018.
Kimsingi mwanafunzi huyo anaesomea uhandisi wa umekanika, ambaye bado ni mwanagenzi, kwa namna fulani alikwepa nadhari ya wakuu wa chama cha waendesha baiskeli cha Uingereza hadi hivi karibuni -- lakini hawezi kupuuzwa tena.
Tanfield alipata ushindi katika fainali ya mbio za mita 4,000 katika uwanja wa Anna Meares Veladrome mjini Brisbane siku ya Ijumaa, na kuongeza medali ya dhahabu juu ya ile ya fedha alioipta saa 24 kabla ya hapo.
Post a Comment