Nsajigwa afunguka NA KUSEMA SIMBA WA SINDIKIZAJI
Kocha Msaidizi wa Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Shadrack Nsajigwa amefunguka na kudai matokeo waliyoyapata katika mechi yao ya jana Aprili 22, 2018 dhidi ya Mbeya City sio kigezo cha wao kuhofia pambano linalofuata na vinara wa ligi Simba SC.
Nsajigwa amebainisha hayo ikiwa zimebakia takribani siku 6 kuelekea mechi yao ya watani wa jadi ambayo imekuwa ikitolewa ndiyo mchezo pekee kila mpenda soka amekuwa akiuotolea macho kujua nani ataibuka mpambe mbele ya mwenzake katika mtufuano huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 29, 2018 katika dimba la Taifa Jijini Dar es Salaam.
"Mechi ya derby ni derby tu haijalishi timu imefanyaje katika michezo yake iliyopita kwa hiyo ni mechi ambayo tuna siku nyingi za kujiandaa kwa hiyo tutajua namna ya ku-plan katika kupambana dhidi ya Simba", amesema Nsajigwa.
Yanga inatarajiwa kushuka dimba la Taifa huku wakiwa na alama 48 kibindoni katika mechi 23 huku wakiwa wamezidiwa alama 11 na watani wao wa jadi Simba SC wenye pointi 59 za mechi 25.
ANGALIA HAPA SYLAS TV
Post a Comment