wabunge 100 ni darasa la saba – Mbunge Msukuma
Mbunge wa Geita Vijijni, (CCM) Joseph Msukuma ameitaka Serikali kuwarudisha kazini watumishi wa umma waliofukuzwa kwa kuwa wana elimu ya darasa la saba hadi watakapostaafu.
Msukuma ameyasema hayo ijumaa hii alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/19.
“Wabunge wenzangu, tuwatake Serikali wawarudishe kazini hadi hapo watakapostaafu. Hapa bungeni wabunge kama 100 hivi ni darasa la saba, wengine wamefeli, wengine wana vyeti feki,” amesema.
Amesema iwapo hawatawarejesha watumishi hao basi wawafukuze hata wabunge ambao wana elimu hiyo au wabunge hao warejeshwe kuwa wa viti maalum.
Post a Comment