Header Ads

China imesema itaanza kutoza ushuru bidhaa za nyama ya nguruwe


Image result for China

China imesema itaanza kutoza ushuru bidhaa za nyama ya nguruwe na matunda zinazoingia nchini humo kutoka Marekani kuanzia leo Jumatatu, hilo likiwa jibu la Beijing kwa ushuru mpya uliotangazwa na utawala wa Rais Donald Trump dhidi ya bidhaa kutoka China. 

Kwa wiki kadhaa, China imekuwa ikitishia kuchukua hatua kama hizo, katika mzozo wa kibiashara unaozidi kupanuka kati yake na Marekani. Ushuru mpya utalenga bidhaa 128 zinazoagizwa kutoka Marekani, na bidhaa nyingine 8 kutoka Marekani, zikiwemo nyama ya nguruwe, zitaongezewa ushuru kwa asilimia 25. 

Bidhaa nyingine 120 kutoka Marekani, zikiwemo za matunda, zitaongezewa ushuru kwa kiwango cha asilimia 15. China ndio mwagizaji mkubwa wa nyama ya nguruwe kutoka Marekani, ambapo mwaka jana pekee iliagiza nyama hiyo yenye thamani ya dola bilioni 1.1.

 Rais Trump aliweka ongezeko la asilimia 25 la ushuru kwa bidhaa za chuma zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, na ongezeko jingine la asilimia 10 kwa bati inayotengenezwa nchini China.

No comments