Header Ads

Mpalestina 17 wapoteza maisha


Image result for Mpalestina mwingine amefariki kutokana na majeraha


Mpalestina mwingine amefariki kutokana na majeraha aliyoyapata siku tatu baada ya kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya umma katika ukanda wa Gaza yaliyokumbwa na vurugu.

 Wizara ya afya ya Gaza imesema idadi ya waathiriwa sasa imefika watu 17. Zaidi ya watu 1,400 walijeruhiwa katika maandamano hayo ya Ijumaa, yaliyoshuhudia maelfu ya watu wakishiriki. 

Umoja wa Ulaya na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka uchunguzi huru kufanyika kuhusu matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji hao. Israel hata hivyo imewatetea wanajeshi wake ikisema wanajeshi hao waliwafyatulia risasi waandamanaji pale ilipohitajika baada ya kudai kurushiwa mawe, mabomu ya kujitengezea na magurudumu ya gari. 

Israel inalishutumu kundi la Hamas ambalo linadhibiti ukanda wa Gaza kwa kutumia maandamano hayo kujaribu kufanya mashambulizi Israel.

chanzo dw swahili

takukulu mkoa wa tabora waokoa milioni miamoja


No comments