Header Ads

Jeshi la Israel limethibitisha uhalali wa video ambayo inawaonyesha wanajeshi wakisherehekea baada ya kumpiga risasi Mpalestina katika mpaka wa Gaza

Image result for Jeshi la Israel


Jeshi la Israel limethibitisha uhalali wa video ambayo inawaonyesha wanajeshi wakisherehekea baada ya kumpiga risasi Mpalestina katika mpaka wa Gaza. 

Mawaziri kadhaa wa Israel, akiwemo waziri wa ulinzi Avigdor Lieberman, wamewatetea wanajeshi walioonekana katika video hiyo, wakati jeshi limesema kuwa Mpalestina huyo alipigwa risasi mguuni na kujeruhiwa. 
Haikubainika wazi kama muathiriwa huyo alifariki dunia.

Jeshi pia limedai kuwa tukio hilo lililotokea Desemba mwaka jana kufuatia maandamano na onyo kutoka kwa wanajeshi. Video hiyo imetolewa katika wakati ambao jeshi la Israel linakabiliwa na uchunguzi wa kimataifa kutokana na matumizi ya yake ya risasi za moto katika mpaka wa Gaza. Karibu Wapalestina 31 wameuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa kufuatia kuzuka kwa maandamano na vurugu katika mpaka huo tangu Machi 30.


CHANZO DW KISWAHILI


ANGALIA VIDEO HI


No comments