Header Ads

jalada limefungwa Askari waliokamatwa tukio la AKWILINA wa pohuru

Leo April 2018 Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu ameonya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.
Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.
“Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.” -Biswalo
Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”
“Niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.” -Biswalo
ccm kutamba tabora angalia hapa

No comments