Viongozi mbalimbali barani Afrika na watu mashuhuri duniani, wanaendelea kutuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha mwanaharakati Winnie Mandela
Viongozi mbalimbali barani Afrika na watu mashuhuri duniani, wanaendelea kutuma risala za rambirambi kufuatia kifo cha mwanaharakati Winnie Mandela, aliyepinga utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
Winnie aliaga dunia jana akiwa na umri wa miaka 81. Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema Winnie alikuwa mwanamke shupavu na imara katika harakati za ukombozi wa Afrika Kusini. Ramaphosa ameendelea kusema.
"Winnie Mandela ameacha urithi mkubwa na kama tusemavyo katika utamaduni wa kiafrika, Mti mkubwa umeanguka. Amekuwa miongoni mwa wanawake shupavu na katika mapambano yetu, aliyeteseka sana chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi, aliyefungwa jela, aliyezuiliwa na aliyedhalilishwa vibaya mno." Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobeli Askofu Desmond Tutu, amesema Winnie Mandela alikataa kusalimu amri hata wakati mume wake wa wakati huo, hayati Nelson Mandela, alipokuwa jela.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema umoja huo unaungana na bara la Afrika kuomboleza kifo cha Winnie ambaye siku zote atakumbukwa kama mwanaharakati asiye na woga na aliyejitolea maisha yake kwa ajili ya kupigania uhuru wa Afrika Kusini na wanawake kote duniani.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema Winnie alikuwa mwanamke mwenye ujasiri usio wa kawaida, aliyesimama imara na aliyeuwasha mwenge wa vita dhidi ya ubaguzi.
tabora amani ya tawara
Post a Comment