Jeshi la Mali limesema, washukiwa 14 wa Jihadi waliuawa
Jeshi la Mali limesema, washukiwa 14 wa Jihadi waliuawa jana, kufuatia kile kinachodaiwa kuwa walijaribu kutoroka kizuizini, siku moja baada ya wao kukamatwa.
Hata hivyo maafisa wawili wameliambia shirika la habari la AFP kwamba, raia 20 waliuawa au walikamatwa Dioura-eneo la kati ya Mali, na hivyo kuibua mashaka kuhusu ukweli wa madai ya jaribio la kutoroka jela.
Mnamo Jumanne, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, liliwataka maafisa wa Mali kuchunguza visa vya mauaji ya kiholela, baada ya kaburi la pamoja lenye miili sita kugunduliwa.
Mali ambayo awali ilikuwa mhimili wa demokrasia na utulivu barani Afrika, imegubikwa na mapinduzi, vita vya wenyewe kwa wenyewe na mashambulizi kutoka kwa makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu.
tabora amani ya tawala
Post a Comment