Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza ametoa motisha ya shilingi laki tatu kwa wachezaji wa Lipuli FC
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Amina Masenza ametoa motisha ya shilingi laki tatu kwa wachezaji wa Lipuli FC muda mfupi kabla ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba SC kuanza kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.
Taarifa ya Lipuli FC imeeleza kuwa kiasi hicho cha pesa kimekabidhiwa kwa kocha msaidizi wa timu hiyo Suleiman Matola ambaye leo akiwa na kocha mkuu wa Lipuli Amri Said wataiongoza timu hiyo kukabiliana na Simba.
''Abuu Sillia akabidhi kiasi cha shilingi laki 3 kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza kama motisha kabla ya mchezo dhidi ya Simba SC''. imeeleza taarifa hiyo.
Kitu cha kuvutia kwenye mchezo wa leo ni kurejea kwenye uwanja wa Samora kwa mlinzi wa Simba raia wa Ghana Asante Kwasi ambaye mzunguko wa kwanza alichezea Lipuli FC kabla ya kusajiliwa Simba kwenye dirisha dogo.
Asante Kwasi pia ndiye alikuwa kinara wa mabao ndani ya Lipuli FC, ambapo alikuwa amefunga mabao matano katika mzunguko wa kwanza huku bao moja kati ya hayo alilifunga dhidi ya Simba kwenye mchezo wa raundi ya Kwanza uwanja wa Uhuru Dar es salaam.
njisi ya kulima shamba kubwa kwa muda mfupi
Post a Comment