Jeshi la Israel limewaua Wapalestina 7 kwa kuwapiga risasi, na wengine 1,070 wamejeruhiwa
Jeshi la Israel limewaua Wapalestina 7 kwa kuwapiga risasi, na wengine 1,070 wamejeruhiwa, wakati wa maandamano yaliyofanywa jana na maelfu ya Wapalestina karibu na mpaka wa ukanda wa Gaza, huku wengi wakichoma matairi na kutupa mawe.
Baadhi ya vyombo vya habari vimemnukuu balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa akisema idadi ya waliouawa ni 9. Kijana mwenye umri wa miaka 16 ni miongoni mwa waliouawa. Aidha, mwanamke mmoja na watoto ni kati ya wale waliojeruhiwa pamoja na waandishi wa habari wa Palestina. Tangu Ijumaa ya wiki iliyopita, Wapalestina 29 wameuawa kufuatia taharuki katika mpaka huo, na watu 2,500 wamejeruhiwa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na viongozi wengine wametaka uchunguzi huru kufanywa kuhusu mauaji hayo.
Maafisa wa Israel wametetea hatua walizochukua kwa kusema baadhi ya Wapalestina waliouawa waliwafyatulia risasi wanajeshi wake, na baadhi yao walikuwa wana mafungamano na kundi la Hamas. Wapalestina hao wanafanya maandamano ya wiki sita kupinga mzingiro wa mpakani ambao umedumu kwa muongo mmoja sasa.
miloni miamoja kuokolewa tabora
Post a Comment