Wanajeshi saba wa Myanmar wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi
Wanajeshi saba wa Myanmar wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi na kazi ngumu katika gereza moja la eneo la mbali baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya kiholela ya wanaume kumi wa jamii ya Waislamu wa Rohingya.
Taarifa ya mkuu wa jeshi la Myanmar imesem wanajeshi hao saba, miongoni mwao maafisa wanne, walihukumiwa chini ya kipengele cha 71 cha sheria ya jeshi nchini humo kwa sababu Warohingya waliouawa hawakukamatwa na kuadhibiwa kwa kufuata utaratibu. Serikali ya Myanmar ilikiri Januari kuwa wanajeshi wake, pamoja na wanakijiji wa dini ya Budha katika jimbo la Rakhine, waliwauwa wanaume 10 wa Rohingya mwezi Septemba mwaka jana.
Tukio hilo lilikuja kama sehemu ya msako mkali wa jeshi la Myanmar dhidi ya jamii hiyo ya waislamu walio wachache, ambayo ilisababisha Warohingya 700,000 kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh.
TABORA TPT KUITAM,BA
Post a Comment