TIMU ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar imetwaa ubingwa
TIMU ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar imetwaa ubingwa wa mashindano ya Muungano baada ya kuifunga Karume Market ya Dar es Salaam kwa penalti 6-5 katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Bandari, Temeke.
Karume Market ambao ni mabingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam walianza kupata bao lililofungwa na Eddy Ngalambe na kudumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko ambapo Jang’ombe Boys ilianza kuliandama lango la Karume Market huku wakipigiana pasi moja moja na kupata bao kwa mkwaju wa penalti lililofungwa na Mustafa Hassan na kufanya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 1-1 na kulazimika kupigiana penalti.
Karume Market ilipiga penalti saba na kupata tano na Jang’ombe walipiga sita na kukosa moja na kufanya waibuke mabingwa kwa penalti 6-5.
Akizungumza kabla ya kukabidhi kombe Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Almas Kasongo alisema mashindano ya Muungano ni mwanzo wa kuendeleza mahusiano ya kisoka kwa Zanzibar na Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mapema mwaka huu tumekubaliana na ZFA kuwa na mashindano ya Muungano na leo hii tumeanza utekelezaji wake na lengo la mashindano ni kuendeleza mahusiano ya kisoka na wenzetu wa Zanzibar ndio maana hapo unawaona viongozi wa ZFA,” alisema Kasongo.
Fainali hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwepo wenyeviti vya vyama vya soka Ubungo, Temeke, Ilala pamoja na wajumbe wa kamati mbalimbali za DRFA na wengine toka Zanzibar.

Post a Comment