Uingereza yawatahadharisha raia wake maandamano
ikiwa wewe ni raia wa Uingereza na unapanga kusafiri kuelekea Tanzania wiki hii unatakiwa kuwa mwangalifu ili kuhakikisha kuwa haujipati katika maandamano ya kisiasa yanayopangwa kufanyika tarehe 26 Aprili .
Katika tahadhari ya usafiri iliotolewa na ubalozi wa Uingereza, wasafiri wameonywa kwamba ijapokuwa safari za kuelekea taifa hilo hazina matatizo yoyote, wageni wanaoingia nchini humo siku hiyo wanafaa kuwa makini kwani iwapo kutakuwa na maandano kunaweza kuwa na 'maafa'.
Kulingana na gazeti la The Citizen Tanzania, tahadhari hiyo ilitolewa kufuatia wito wa kufanyika kwa maandano dhidi ya serikali na mwanaharakati wa mtandaoni anayeishi nchini Marekani Mange Kimambi.
Anadai kwamba maandamano hayo ni ya kupinga ukandamizaji wa uhuru wa kisiasa na unyanyasaji wa haki za kibinaadamu.
Serikali tayari imepinga madai hayo na kusema kuwa maandamano hayo yatakuwa kinyume na sheria.
Rais John Magufuli amesisitiza kuwa maafisa wa usalama watakabiliana na wale watakaoshiriki katika maandamano hayo.
''Kutokana na uzoefu wa hapo mbeleniu balozi wa Uingereza nchini Tanzania umeonya kwamba maafisa wa usalama nchini Tanzania huenda wakatumia vitoa machozi na hata risasi kukabiliana na mandamano yoyote haramu''.
''Kuweni makini mulipo na epukeni makundi makubwa ya watu ama maandamano ya umma'', ilisema taarifa hiyo.
Takriban raia 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila mwaka.
Post a Comment