Ufaransa imesema italipiza kisasi dhidi ya utawala wa Syria
Ufaransa imesema italipiza kisasi dhidi ya utawala wa Syria wa Rais Bashar al-Assad iwapo kutatokeza ushahidi kwamba ulihusika na kile kinachoshukiwa kuwa ni shambulio la gesi ya sumu ya klorini katika eneo linalodhibitiwa na waasi.
Msemaji wa serikali ya Ufaransa Benjamin Griveaux ameiambia Redio Europe nambari moja, kwamba taarifa za upelelezi za Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Donald Trump wa Marekani zinaashiria silaha za kemikali zilitumika.
Viongozi hao wawili walizungumza kwa simu jana usiku kuhusu shambulizi la kwenye mji wa Douma Jumamosi iliopita ambapo zaidi ya watu 40 waliuwawa katika kile kinachotajwa kuwa ni shambulio la gesi ya sumu.
milioni miamoja kuokolewa
Post a Comment